sponsor

sponsor
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Slider

Contact us

Videos

Technology

Comedy / Vichekesho

Kiswahili Section

Knowledge zone

Entertainment

Je wajua

» » » » » Chapter 1 of Group Admin by Yuster Anyimike
Sura ya kwanza

Miezi mitatu ilikuwa imepita tangu nianze kazi katika kampuni ya…………… nilimtazama mfanyanyakazi mwenzangu aliekuwa akicheka na simu, tulimuita dada jane .nilitamani kujua alikuwa anachekeshwa na nini lakini nilishindwa sikuwa nimemzoea, wengi waliniita mpole na mkarimu, neno hapana halikutoka mdomoni kwangu pale niliombwa msaada, aibu yangu ilinifanya niwe na marafiki wachache sana hasa wakiume, wafanyakazi wenzangu walipenda kunitania hicho kilinifanya mda mwingi niwe bize na kazi. Nilimwangalia tena dada Jane alitingwa Sana safari hii alicheka na kufuta machozi nilijikuta nacheka pia, niliendelea na kazi niliokuwa naifanya 

“Penny” dada Jane aliniita 

“Sikuoni kwenye group la ofisini, hutaki kujiunga? Yaani unakosa mambo mengi saana, nikunganishe?” Nilimtazama dada Jane na kutabasamu, alinikumbusha magruop yangu ya whatsapp nilimuelewa, nilimjibu kuwa ningefurahi kuunganishwa, alininiahidi admin akirejea atatuma namba yangu, gafla alianza kunielezea sifa za group na mifuko iliyopo 

‘Nani group admin?’’ nilijikuta nauliza.kabla hajajibu simu ya mezani kwake iliita aliipokea na kutoka, nilihuzunishwa kidogo lakini nilijua nitawajua wote nikiunganishwa. Muda wa kazi ulipita nilitoka ofisini kuelekea nyumbani nilipitia dukani kununua vifaa vyakupikia pamoja na vocha ,nilifika nyumbani na kukuta giza kama kawaida ikifika zamu ya mama mwenye nyumba kununua umeme tatizo hutokea,nilijikuta nahapa kuhama nyuma hiyo mwezi ujayo sikujali miezi miwili iliyo baki ya kodi yangu ,kero za wapangaji zilinichosha.nilihairisha kupika, na giza nilikunywa maziwa baada ya kuoga na kujirusha kitandani niliweka vocha na kujiunga kifurushi.niliona group la kazini walionekana wacheshi,wachache niliwaona kwa sura wengine nilikuwa siwajui kabisa ,nilikaribishwa vizuri,gafla mfanyakazi mmoja alisema anatafuta mchumba,mwanachama waliokuwapo walicheka sana sikutilia mkazo maneno yale,walijitambulisha na idara walizotoka,walimuita admin ajitambulishe idara aliyotoka,apo niliweza kujua kwanini walicheka sana yule mfanyakazi aliposema anatafuta mchumba ndie aliekuwa group admin akitoke idara ya ukaguzi (auditing).baada ya nusu saa watu walitawanyika kwenda kulinda ndoa zao,ambao hamjaolewa mnaweza kuendelea,mfanyakazi mmoja aliongea,tuliokuwepo tulicheka tena,maongezi yaliendelea sikuweza kuongea sana kwasaabu ya ugeni wangu,mara nyingi admin alinisihi niongee nisiogope ila sikuweza nilijiuliza ni kweli admin hajaoa ? Niliona utani kwanza haikuwa inanihusu, usingizi ulinipitia, nilishtushwa na milio ya ujumbe wa maneno zikiingia, magruop mengi nilitoa sauti nilivuta simu yangu kuangalia wakina nani wako macho, nilikuta admin na wengine. Nilizima simu na kulala..siku zilipita niliaanza kulizoea group sikuwa muongeaji sana ila nilifuatilia kila kitu, nilijua nani muongeaji sana nani mcheshi, sukuwajua kwa sura kawasababu wachache sana waliweka picha zao……… lakini kimajina niliwajua kwa kiasi cha kuridhisha,niliamini nitakutana nao wote sikumoja.Aibu yangu ilipungua siku hadi siku niliunda marafiki pia wanawake kwa wanaume,bila kumsahau dada jane alikuwa mshauri wangu mkubwa hasa pale wavulana walipoanza kunitaka kimapenzi,nilifanikiwa kuhama nyumba ya mwanzo nashukuru nilipata mahali pazuri na karibu na ofisini nilitumia nusu saa tu kutoka ninapoishi mpaka kazini. Kama kawaida inapofika saa saba wafanyakazi wote hutoka maofisini kwenda kupata chakula cha mchana ,siku ya leo ilikuwa tofauti hali ya hewa ilikuwa si shwari dalili ya mvua ilionekana kwa mbali nilijilaumu kwa nini sikutembea na mwamvuli ila nilijipa moyo huweza mvua isinyeshe, nilishuka taratibu kuelekea kwenye mgahawa gafla mvua ilianza kunyesha niligeuka ili nirudi ndani niligongana na mtu aliyenikinga na mwamvuli,nilisimama kuinua uso kumtazama ni nani nilikutana na sura ngeni,nilimwangalia kwakuvuta kumbukumbu kama namfahamu hakuingia akilini,nilihisi labda ni mkurugenzi mwenyewe,ila nilipingana na hilo wazo hakuwa mtu mzima kwa haraka haraka nilihisi amenizidi miaka si juu ya mtano ,katika umri wangu huu wa miaka 25,alikuwa kijana mzuri, mwenye sura ndefu kichwa chake kilihifadhi nywele fupi kilichonyolewa vizuri ,alionekana nadhifu kwa jinsi alivyokuwa amevaa , harufu ya marashi yake ilinipitia puani mwangu, alitabasamu baada yakuniona nikimshangaa,tabasamu lake lilifanya mapigo ya moyo wangu yaende mbio,mvuto wake uliongezeka mara mbili, alinionyeshea ishara ya nianze kutembea taratibu niliinua mguu kuelekea mgahawani,nilijikuta najivuta mbali naye nilijiona sifai kumsogelea karibu 

“Unalowanisha nywele zako, sogea karibu”aliongea na kunisogeza karibu, kimya tulitembea mpaka kwenye mgahawa, alitafuta sehemu na kuketi .nilibaki nimesimama sikutaka kukaa pembeni yake niligeuka kutafuta meza nyingine 

“Penny” yule kijana aliniita, niliashangaa amejulia wapi jina langu sikuwa nuimevaa kitambulisho cha kazini, niligeuka kumuitikia alinikaribisha kwenye meza kwauoga niliketi 

“Najua utakuwa unashangaa nimekujuaje, nawajua watu wangu wote’’ aliongea yule kijana, sikumuelewa alimaanisha nini, nililazimisha tabasamu 

“ nitasikitika kama humfahamu admin wako penny,usijitetee kuwa ni mgeni,” aliongea huku akitabasamu nilitamani kumwambia asitaasamu lakin nilishindwa,ila moyoni nifurahi kumuona admin kwa mara ya kwanza,hakuwa mcheshi tu bali na uzuri pia,waswahili usema hakuna mwanaume mzuri ila mimi nasema admin ni mzuri,nilimwangalia alipokuwa anaongea na mhudumu tabasamu halikukauka usoni mwake,aliongea kwa nidhamu na kwa upole , aligeuka kuniuliza nakula nini,niliagiza ndizi za kukaanga na mishikaki,admin aliagiza ndizi samaki, “Niambie penny, ni kweli ulikuwa hunifahamu,’’ aliongea na kuusogeza uso wake karibu yangu nilijikuta narudi nyuma haraka.alicheka na kurudi “Iangalie vizuri hii sura husiisahau tena sawa,” sikuweza kujibu Zaidi ya kutabasamu, aliinama chini kujibu ujumbe ulioingia kwenye simu yake 

“Unaniangalia,” aliongea akiwa bado ameinama.nilishtuka Kwa aibu, niljiona mjinga kwanini nilishindwa kujizuia kumtazama admin 

“Mimi? ‘’ niliuliza kupoteza muelekeo 

“ ndio wewe,kuna mwengine Zaidi yako,usiwaze nimeshazoea kutazamwa ,wanasema mimi mzuri,eti ni kweli,ukinijibu wewe nitaamini” safari hii aliinua uso wake kunitazama sura ilibadilika kidogo 

“ wanasema na uwezo wa kumpata msichana yoyote ninaye mtaka,napingana nao kila siku,nijibu wewe labda nitaamini”.nilimwangalia tena na tena.nilitaka kumuambia sijawahi kukutana na mvulana mzuri kama wewe,mcheshi ,nadhifu,machapakazi,mwenye moyo wa huruma,msichana yoyote angejivunia kuwa na wewe,lakin 

Maneno hayakuthubutu kutoka kinywani mwangu “ kwa jinsi unavyoniangalia naanza kuamini maneno yao,au kuna lingine unashangaa ,eti mama”.nilipenda alivyoniita mama wengine hawakuwahi kunipa heshima kama hiyo admin ni mtu wa aina gani,nilizidi kuchanganyikiwa,nilimshukuru mhudumu alileta chakula angalau niliweza kutoa macho yangu kwa admin na kuyaweka kwenye chakula,aliniongelesha mambo mengi kuhusu mazingira ya ofisini,alikuwa na miaka sita tangu aanze kazi apo,nilimpongeza kwa zawadi za ufanyakazi bora alizokuwa anazipata kila mwaka,sikuwahi kuwaza kama duniani kuna watu waliokamilika kama hivi,nilitamani kujua kuhusu maisha yake mwenyewe ila nilijipa moyo ipo siku nitayajua tuu,tulimaliza chakula na kuanza kurudi ndani, tukiwa tunakaribia kupanda ngazi,kwa sauti ya upole admin aliniita,niligeuka kumtazama,alinisogelea karibu mpaka sikioni mwangu nilihisi naishiwa nguvu, amenipenda!! Moyo wangu alilipuka nilitamani nimjibu I love u too kabla hata hajasema.nilianza kuona mapigo ya moyo yakienda mbio, 

‘ 

“ funga kifungo cha shati kimefunguka” alininong’oneza ,nilijikuta nashunza pumnzi,maskini penny hili wazo la kupendwa na mtu kama admin lilitoka wapi,sikuwa nastahili hata kuongozana nae ,basi tu moyo wake wa ukarimu haukuweza kuona tabaka kati yetu,alirudi nyuma nakuanza kuondoka 


-----------------------------------------------------------------------------------------------------

                                                                                      Imetungwa na Yuster Anyimike

Inaendelea 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post