sponsor

sponsor
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Slider

Contact us

Videos

Technology

Comedy / Vichekesho

Kiswahili Section

Knowledge zone

Entertainment

Je wajua

» » » » » Chapter 2 of Group Admin by Yuster Anyimike


Sura ya Pili

“Admin asante” nilimwambia 

“Niite Nathan” aliongea na kuondoka.nilisimama pale njiani kama dakika tano nikitafuta nguvu ya kutembelea, nilifika ofisini na kuketi niliona macho ya kila mtu yakinitazama, nilidhani vifungo vimefunguka tena nilijiangalia lakini niliona niko salama “Naona penny Leo umebahatika kula na nathani “dada jane aliamua kuvunja ukimya, wengine walicheka “eti tuambie mliongea nini,kuna kitu alikunong’oneza sikioni ilikuwa nini?’’ alitania jirani yangu wa meza “Mmh sasa James mpaka vya skioni unavitaka’’ alimalizia dada jane naz wengine wakacheka huku wakiniangalia, mda wote huo ckuweza kujibu kitu Zaidi ya kutabasamu kwa aibu, “Naona ni siri hataki kujibu, haya bana, mimi sisemi sitaki kuitwa mbea, kwa macho yako utaona’’ dada Jane aliongea na kuendelea na kazi 

‘ asikutishe mwaya penny,tabia ya admin inajulikana sana ,hatujamzoea sana ila…..’’ james alisjindwa kumalizia baada ya mkurugenzi kuingia,aliongea nasi kwa mda wa dakika mbili na kuondoka kulikuwa kuna kikao saa tisa staff wote wa kiwanda kizizima watakuwepo,nilijikuta nafurahi niljua nimepata nafasi ya kumuona admin kwa mara nyingine,kila wakati niliangalia saa ,mda sikuona ulipitaje hatimaye saa tisa ilifika,nilifunga vitu vyangu na kuelekea maliwatoni, niliweka vizuri nguo zangu na kubana mywele upya,kilikuwa kikao cha kwanza kikubwa tangu nifike ofisi hiinilitaka kujua kama kuna wakina Nathan wengi kwenye hii kiwanda,niliingia ukumbini na kuketi mahali,macho yangu yalipapasa huku na kule kumtafuta admin lakin sikufanikiwa,moyo ulianza kuhuzunika. Mara nilimuona mkurugenzi mkuu akiingia ukumbini akiongozana na admin huku wakicheka, cheko alke liliusuhuza moyo wangu, nampenda admin! Moyo ulitamka rasmi kichwa kikakubali mwili ukasisimka kwa mara nyingine,sikujua upendo huo umeanza leo au lini haikuwa na umuhimu kwangu, moyo wangu ulijua kiasi gani unamuhitaji,niliinama chini kusoma ajenda za kikao ,mkutano ulianza rasmi nilisikitika kuwa sehemu niliokaa sikuweza kumuona admin vizuri ila nilifarijika baada ya kusikia mkuregenzi akimtambulisha kama mkaguzi mkuu wa kiwanda hiko,alisimama kutoa ripoti ya miezi sita ya ukaguzi wake,niligundua kuwa sikuwa mimi tu nilie kuwa nikimtazama admin kwa macho tofauti,wasichana wengi walionekana kumtazama,wengi walikuwa warembo Zaidi yangu ilinikatisha moyo,nilijitahidi kurudisha mawazo iliniweze kusikiliza ripoti yake lakini sikuweza,sura yake ilinipitia usoni sauti yake ikininong’oneza sikioni harufu ya marashi yake hivyo ndo niliweza kuvielewa ,mikono yake begani mwangu huku akiniambia nisogee karibu yake nitalowa na mvua vilinijia tena, nilishindwa kujielewa nimekamatwa na nini safari hii.alimaliza kutoa ripoti yake na kuketi wakuu wengine wa idara walitoa ripoti zao pia.kikao kiliisha sikutaka kuongea na mtu niliaga waliokuwa karibu yangu na kuelekea mlangoni niligeuka mara ya mwisho kabla ya kutoka nje macho yangu yaligongana na admin alitabasamu na kuendelea kuongea na mfanyakazi aliekuwa pembeni yake, mapigo ya moyo yaliongeza kasi nilitoka nje kwa haraka kuelekea kituo cha magari.moyo wangu hukuwahi kumpenda mtu kiharaka hivyo ulichukua mda kumsoma na kumuelewa kabla ya kupenda, kimetokea nini kwa admin? Ni swali lililo kosa jibu. Nilipanda gari na kurudi kwangu sikutaka kukipa kichwa changu mda wa kufikiri.nilipika chakula na kuandaa nguo zangu za kesho kazini,niliingia bafuni na kujirusha kitandani baada ya kumaliza,nilichukua simu kuwa salimia marafiki zangu hasa emmy nilitamani nimwambie yaliyonisibu ila nilijua lazima emmy angenicheka ,nilisalimia magroup yangu niliyokuwa nayo,kasoro la kazini lilikuwa kimya,kabla sijatoka admin aliaga usiku mwema kwa wanachama wake,niliogopa kujibu nilisoma nakutoka,baada ya dakika mbili sms iliingia kwenye simu moyo ulishtuka kuona imetoka kwa admin, 

“nakuona ukomacho penny, na wewe unatatizo la kulala kama mimi, anyway usiku mwema’ 

Nilibaki nikitazama ile sms kwa mda,sikujua nijibu vipi ,nikubali ili tuendelee kuongea au niache aondoke,niliamua kutojibu.nilizima simu na kulala.siku zilienda haraka wiki lilisha bila kuliona,mara nyingi nilimuona admin kwa mbali sikuweza kumsogelea niliogopa macho ya watu,niliishia kumtazama kwa mbali,mara mbili nilikutana nae mlangoni tulisalimiana na kila mtu kuendelea na shughuli zake,muda mwengine nilijikuta natamani nimwambie ukweli kuhusu hisia zangu lakini nilisita atanielewa vipi,pili sistahili kuwa nae, nilibaki nalo rohoni,nilisema nibadili kila kitu changu kwanza ,labda nitaweza kumpata,nilibadili nywele nilianza kutumia mitindo tofauti,nilikuwa makini hata kwenye kuvaa umbo langu la kihaya lilianza kuonekana .niliwaona jinsi wavulana walivyokuwa wakinitazama moyo wangu haukuridhika sio wao niliokuwa nawataka,nilie muhifadhi moyoni alionekana kutingwa na kazi,nilihuzunika sikuona maana ya kufanya yotehayo bila matunda yoyote,. 

Ilikuwa siku ya ijumaa nikiwa nimevaa gauni jipya kabisa.nilijiangalia mara mbili mbili na kujikubali, natoka mlangoni mpangaji mwenzangu aliniona na kunisifia kichwa changu kiliongezeka ukubwa, hakika nilipendeza. Niliingia ofisini nilichotegemea nilikipata ,maneno kutoka kwa james na dada jane,nilicheka sana hasa dada jane aliponiambia nisipopewa lift leo sitakaa nipewe tena maishani,akili yangu ilielekea kwa admin niliomba mungu nikutane nae leo. Mda wa chai ulifika nilikuwa wa kwanza kutoka nje moyo ulifurahi baada ya kumuona admin akishuka kutoka kwenye gari lake kuelekea mlango niliokuwa nimesimama ,alinifikia na kunisalimia akaingia ndani tabasamu la kila siku halikuwepo usoni mwake ,hata usoni hakuniangalia,niliumia sana,sikuamini nilichokiona ,nilijikuta natoa tabasamu nililoambatana na maumivu nilitembea taratibu kuelekea mgahawani nilitafuta meza ilijificha na kukaa ,sikutaka kufikiri kilichotokea,njaa ilipotea gafla nilinyanyuka na kurudi ndani,nilikaa kwenye kiti changu,sms ziliingia kwenye simu niliichukua simu na kuiweka kwenye droo.niliona dada jane akiniangalia “Vipi wewe, mara hii umekunywa chai?’’ aliongea nhuku akikusanya vitu vyake kujiandaa kwenda kunywa chai 


“ nimegairi tumbo langu limejaa gafla,nitakula cha mchana” niliongea na kunyanyuka ,dada jane alibaki akinitazama alionekana anataka kuuliza swali ila niliondoak kuelekea maliwatoni,nilifika mbele ya kioo na kujitazama nilfuta kila kitu nilichokuwa nimepaka usoni niliosha uso kabisa ,na kurudi ofisini,nilitafuta viporo vyote vya kazi nilivyokuwa navyo na kuzifanya.mara kwa mara sura ya admin ilinipitia kichwani nilijitahidi kuipoteza,niliskia sauti ya james ikiniambia mda wa chakula cha mchana,nilimwambia atangulie nakuja,sikutaka kutoka nje,ila njaa ilikuwa kali,nilinyanyuka kwenda nje,nilitafuta meza iliyojificha na kuketi ,chakula nilichoagiza kilikuja,kwa mda wa dakika tano nilibaki nikikitazama kile chakula 

“Nikusaidie inaonekana huna njaa” sauti ya kiume iliniongelesha, niliuinua uso kumtazama, admin! Alitabasamu na kuketi 

“Hujanikaribisha” alitania, kwasauti ya upole nilimkaribisha, niliona miguu yangu ikitetemeka sikujua ni kwanini, nilinyanyua glass yangu yangu ya maziwa na kunywa 

“Inaonekana unapenda maziwa ya mtindi, mara nyingi nakuona ukiyatumia” neno mara nyingi lilinipa faraja, 

“Huwa unanichunguza na kula nini admin” niliongea kwa kutabasamu sikujua nguvu ya kuongelea niliipata wapi 

“vipi siruhisiwi?’’ safari hii aliniangalia moja kwa moja kwenye macho nyangu ,niliinama kujificha labda angeweza kusoma hisia zangu,kwanza niliji0na mwenye bahati kuja kwangu na kuruka meza zote zlizokuwapo pale,yale maumivu ya asubuhi yalipotea nilitamani kumuuliza kama alikuwa na tatizo lolote ,lakini sikujua nianzie wapi,nilimtazama alivykuwa anakata chakula kwa upole,niiangalia mikono yake ilionekana laini labda kushinda yangu ,hivi… 

“Unapenda kuniangalia” admin alinikatisha mawazo yangu, maneno yake yalinipa aibu, aliuinua uso wake kunitazama vizuri 

“Uwa unawaza nini ukiniangalia? Natamani kujua unaniwazia nini, maswali Kama yapo niulize?’’ aliongea na kuweka kijiko chini. 

“husiogope niambie tu ,au uwa unawaza niko kitandani na wewe?’’ chakula kilinipalia,alinyanyuka alipokuwa amekaa na kunipiga piga mgongoni alienda kuchukua maji na kunipa kunywa aliketi baada ya kuniona nimetulia, nilgeuka kuangalia watu pembeni nashukuru mungu kila mtu alikuwa katingwa ,
“ nilikuwa nakutania penny ,kumbe muoga hivyo!” 
“ hapana admin,sikutegemea kitu kama hicho kutoka kwako” 

“Nilisema niite Nathan, pili Mimi na nini? Na vinne au?’’ nilijikuta nacheka 

“Kumbe uwa unacheka!! Walishawahi kukuambia kuwa ukicheka unapendeza?’’ maneno yake yalinifanya nicheke Zaidi 

“Basi sikusifii naona unaleta sifa” niliendelea kucheka mwisho nay eye alijiunga kucheka, alinyamaza kuniangalia nikicheka.nilitulia na kumwangalia nilinyanyua maziwa yangu na kunywa 

“Husipende kutumia vitu vya mafuta sana utanenepa” aliongea baada ya kuangalia ugali na mishikaki niliokuwa nakula.niligundua kuwa hapendi watu wanene
“nashukuru mungu huwa sinenepi hata nile nini” 

“Kweli!! Basi unamwili mzuri, lasivyo u…” alikatisha maneno yake alibaki akiniangalia, nilijua alitaka kusema umbo ila alijizuia, nilifurahi kuona admin ananijua hivyo, niliona akisogeza mkono wako karibu yangu na kuushika mkono, mapigo yaliongezeka kasi tena 

“Relax unatetemeka, kwanini huwa unayakwepa macho yangu” 

“Sitetemeki wala kukwepa macho yako” 

“Nayaskia mapigo yako ya moyo, yanaenda kasi, nini tatizo penny” nilitaka kusimama kwamacho yake aliniambia niketi 

‘Ukiondoka kwa hali hiyo watu watajiuliza kimetokea nini kati yetu, nataka nikuambie kitu” 

“Utaniambia baadae” niliongea na kuuchomoa mkono nwangu, nilijuta kwanini mda umeisha nilitamani nimewambie afanye haraka kuniambia ila aibu yangu nilinizuia 

“Nimezaliwa leo, niambie happy birthday, kila mtu ameisahau, nilitaka kutafuta rafiki wa kumkumbusha angalau nimekupata wewe” kwa mara nyingine niliumbuka, hivi nategemea nini kutoka kwa admin? Mara ngapi ananionyesha kuwa sina hadhi nya kuwa msichana wake lakini siskii.ananiona Kama rafiki amelitamka wazi 

“Ulichokuwa unataka kuniambia ni hiko?” nilijikuta nauliza, admin alionekana kuniangalia kwa mshangao, 

“Vipi kuna lingine ulitegemea? Leo umevaa gauni, hakuna kifungo kilicho funguka”aliongea na kusimama, nilijikuta nacheka, 

“Najuta kukuambia ukicheka unapendeza” nalimalizia na kuondoka, aliniacha nikicheka, nilimwangalia akitembea kuelekea ndani, I love you Nathan, moyo wangu ulitamka. .nilishtushwa na mtu akinishika bega 

“Husithubutu Penny, kimbia bado ni mapema “aliongea ilikuwa sauti ya dada Jane, sikuelewa anamaanisha nini.kabla sijamuuliza aliniambia kuwa admin aliandaliwa tafrija fupi na mkurugenzi kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa, 

“Mwambie kabisa mpenzi wako leo utachelewa kurudi nyumbani” aliongea na kuondoka, nilikumuka kuwa sikuwahi kuwaambia ofisini kama naishi peke yangu, nilitabasamu ila maneo ya mwanzo yalinipitia kichwani.nikimbie kwanini? Admin muhuni, au ameathirika? Sikupata jibu sahihi, niliamini mda ukifika nitaelewa alimaanisha nini. Nilirudi ofisini na kuendelea na kazi huku nikiisubiri tafrija kwa hamu.nilishukuru nilivaa nguo nzuri.mda ulifika nilienda bafuni kujiremba upya, nilitoka nakukutana na dada Jane aliniangalia na kucheka. 

“Umependeza, penny mrembo sana, hivi unajijua?” 

“Nipishe uko” niliongea na nilimshika mkono kuelekea nae ukumbini, baada ya dakika kadhaa ukumbi ulizimwa taa, ulipowashwa sauti zilisikika zikiimba happy birthday to Nathan, admin alitabasamu na kuelekea upande wa keki ilipo,alimnong’oneza kitu mkurugenzi kwa mda,alisogea pembeni kuongea na simu,mkurugenzi alituambia tuendelee kupata vinywaji ukutukisubiri mgeni maalumu,macho yangu haya kucheza mbali na admin,maneno yake ya mchana yalinijia kichwani tena,kwa mda nilihama ukumbini nilijiona niko nyumbani kwangu na admin,akiwa jikoni akinisaidia kupika ,nilitazama kifua chake kilichochuruzika jasho, nilinyanyuka na nilimsogelea na 

kumzungushia mikono yangu nilimlalia mgongoni
“ hatuli leo mama” aliongea ,alinigeuza alinipitisha mikono yake kiunoni alininyanyua akaniweka juu kibalaza cha jiko,aliushika uso wangu kwa mikono yake miwili,taratibu aliupenyeza ulimi wake ndani yangu,mikono yake ilihama usoni ilipapasa mgongo wangu,alinibeba kuelekea nami kwenye kochi ,aliniangalia usoni niliinua uso wangu lakini aliukwepa na kuupeleka shingoni mwangu.. 

“penny angalia nyuma” dada jane alinitingisha ,nilitamani nimzabe kibao,kwa hasira niligeuka nyuma,nilikutana na msichana mrembo urefu tulilingana ila uzuri wake sikuufikia hata nusu,mwendo wake ulikuwa wa madaha,gauni alilovaa lilimpendeza sana wanaume wengi walijikuta wakimuangalia 

“Yaan ukimuangalia uwezi ukaamini kama anawatoto wawili, Nathan sijui alimtoa wapi” aliongea dada jane,sikujua alikuwa kuwa anamuongelea Nathan yupi,niligeuka kumuangalia vizuri dada jane 

“Ohoo kumbe humu kuna Nathan wengi ehee?” 

“Nathan group admin!! na wewe mda wote na urafiki na admin hajawahi kukuambia kama ameoa?’’ alimalizia dada jane aliondoka kwenda kufuata vinywaji vengine,nilibaki nimesimama nikishangaa,yule mdada alimfuata admin alipo na kumkumbatia,admin ameoa!!!!...


-----------------------------------------------------------------------------------------------------

                                                                                      Imetungwa na Yuster Anyimike

Inaendelea 


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post